Kuhusu
Huu ni msururu wa mazungumzo yanayoangazia dhana za kimsingi za afya.Hivyo ndivyo twaweza kuishi kwa afya njema. Bila shaka,tunapokuwa na afya bora, hatuhisi tu vizuri bali twaweza kufanya vitu vyema na kufanya kazi nyingi. Hata hivyo, hatimaye sote tuta aga dunia haijalishi kama tutajiweka vizuri ama hata tukijaribu kujitunza kiafya. Zaidi ya hayo, hata katika hali nzuri ya afya, sote hukumbana na mateso. Mateso haya yaweza kuwa ya kimwili au kimawazo au yote kwa wakati mmoja.
Bibilia ina mengi ya kusema kuhusu afya. Kwa hakika mwandishi mkuu wa sehemu ya Agano Jipya alikuwa daktari. Jina lake ni Daktari Luka. Bonyeza hapa kupata maelezo Zaidi kumhusu Daktari Luka.”