Nini ndoto yako?
-
Yeremia 29:11
Close
Pointi Nzuri za Riziki
Katika kipindi cha pili, Riziki anaiba katika mtihani wa hesabu ili apate pointi mzuri. Chokoza anajaribu kumridhisha Bahati ajivunie pesa kwa njia mbaya. Wote wanajifunza Kuhusu kufanya kazi kwa bidii
Wa Kipekee
Katika kipindi cha tatu, Bahati na Riziki wanachekelewa na watoto wengine kwa ajili ya mavazi yao. Wote wanajifunza kuwa wameumbwa vyema na mwenyezi mungu.
Ua Rembo
Katika kipindi cha nne ,Riziki anapokea ua maridadi lakini linaharibiwa na Pendo. Riziki hapa anajifunza kuhusu upendo, msamaha na heshima. Nyanya yao anaaeleza Pendo umuhumu wa kueka msingi bora katika maisha yake.
Master K akuja Nyumbani
Katika kipindi cha tano, Master K ambaye ni bingwa katika kandanda, anakuja kijijini mwa kina Bahati. Bahati anajifunza kuwa maishani kuna vitu vya maana zaidi kuliko pesa na umaarufu
The Golden Rule
Katika kipindi cha tano, Mmoja wa wanaume kijijini mwao anapatikana kuwa anaugua ugonjwa wa virusi vya ukimwi. Wanakijiji wengi wanamkata lakini Juma anamuonyesha huruma.Riziki anajifunza kuwa ni muhimu kutendea watu vile wewe mwenyewe ungelipenda kutendewa.
Chenji Mingi zaidi
Katika kipindi cha saba, wakati Riziki anapokea chenji mingi zaidi kutoka kwa Juma, anaamua kununua ushanga wa shingo na hizo pesa. Riziki anatamani sana kuiweka lakini anajifunza kuwa tabia nzuri ni muhimu zaidi na anaamua kujirekebisha.
Bahati aumia
Katika kipindi cha nane, Bahati anajeruhiwa akicheza kandanda na analazimika kupumzisha mguu kwa muda mrefu. Anapovumilia haya yote, anajifunza mengi kujihusu na anapokutana na shujaa wake master K, Bahati anajifunza kuwa kuna mengi zaidi kuhusu ukubwa kushinda pesa na umaruufu pekee yake.
Pahala pasipokuwa sawa.
Katika kipindi cha tano, Pendo anawakazia Riziki na Malaika kuungana naye wajiuze kwa wanaume. Riziki ana jaribiwa akifikiria juu ya vitu vyote vizuri ambavyo Pendo akonavyo. Malaika anamwelezea ukweli wa mambo. Wote wanatambua ukweli na wanajiepusha kutokana na maovu.
Kupigana.
Katika kipindi cha ya kumi, Pendo kutokana na wivu, anajaribu kuja kati ya Riziki na Malaika kupitia uongo. Wote wawili wanamuamini na baadaye wanajifunza kuhusu upendo na msamaha.
Siku ilionyesha
Katika kipindi cha kumi na moja, Riziki na Bahati wanachoshwa na kukaa kwa nyumba kwasababu ya mvua. Wanapigana na kwa bahati mbaya, wanavunja nyungu ya nyanya. Nyanya anawafunza juu ya nguvu ilio katika maneno na matendo ya watu. Inamlazimu Bahati kuamua vyema anapokumbana na jambo gumu wakati Chokoza anampomkazia kuungana na wakora.